Bondia mmoja aliyepata jeraha la kichwa katika pigano lake la kwanza amefariki.
Kuba
Moczyk mwenye umri wa miaka 22 alipigwa knockout katika raundi ya tatu
katika pigano la siku ya Jumamosi katika ukumbi wa Towe Complex huko
Yarmouth.
Familia yake imesema kuwa alifariki siku ya Jumatano
usiku katika hospitali ya James Paget huko Gorleston,ambapo amekuwa
bila fahamu na kwamba amekuwa akisaidiwa na mashine.
Mkufunzi
wake Scott Osinski amesema siku ya Jumatano kwamba bwana Moczyk alikuwa
anaelekea kupata ushindi kabla ya kupigwa konde hilo lililomuangusha.
Mpinzani wake alikuwa na umri wa miaka 17.
Post a Comment