0

WATAALAMU wa sheria na kanuni za usalama barabarani nchini, wamesema ajali nyingi zinazohusisha vyombo vya moto hazitokei kwa bahati mbaya bali zinachangiwa na makosa yanayofanywa na madereva kwa kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.

Dereva kuendesha chombo cha moto akiwa amelewa, kukosa ujuzi na weledi, ni baadhi ya mambo yanayosababisha matukio mengi ya ajali zinazosababisha vifo na vilema vya kudumu kwa watu wengi.

Mkufunzi wa Sheria za Barabani nchini, Hubert Kubo, alisema jijini Dar es Salaam kuwa madereva wengi wanaosababisha ajali husingizia ubovu wa magari, barabara au makosa ya kibinadamu, lakini wanasahau jukumu lao katika kuzuia ajali hizo.

"Binafsi nimekuwa mwalimu wa sheria za usalama barabarani kwa zaidi ya miaka 20 sasa, ninachoamini ni kwamba ajali karibu zote zikitokea tambua kuwa kuna mtu hakutimiza majukumu yake ipasavyo akiwa barabarani,” alisema na kuongeza:

Post a Comment

 
Top