Kuna wengine wao selfie ndio kila kitu
utafikiri walisoma photojournalism; yani kila mara popote alipo ni
kujitwanga picha wee… na hivi siku hizi kuna powerbank ndio kabisaa
hawahofii kwamba simu itazima.
Sasa taarifa ikufikie wewe mpenda picha za selfie kwamba takwimu za
utafiti uliofanyika hivi karibuni juu ya vifo vinavyochangiwa na upigaji
picha vimekuwa vikiongezeka kila uchwao kwani mwaka 2014 walikufa watu
15, 2015 wakafariki watu 39 na mwaka huu kwa kipindi cha miezi nane ya
awali tayari wamefariki watu 73.
Utafiti uliofanywa na Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu Hemank Lambawa akishirikiana na wenzie wa Chuo Kikuu cha Carnegie Mellon huko Pittsburgh umegundua njia ya kukabiliana na vifo hivyo ni kutengeneza App maalumu itakayokuwa ikitoa ishara mara mtumiaji awapo kwenye hatari ili aweze kujihami.
Tazama baadhi ya picha ambazo watu wamekuwa wakipiga selfie licha ya kuwa kwenye hatari ya kupoteza maisha.Utafiti uliofanywa na Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu Hemank Lambawa akishirikiana na wenzie wa Chuo Kikuu cha Carnegie Mellon huko Pittsburgh umegundua njia ya kukabiliana na vifo hivyo ni kutengeneza App maalumu itakayokuwa ikitoa ishara mara mtumiaji awapo kwenye hatari ili aweze kujihami.
Post a Comment