0

 Baadhi ya wahitimu wa elimu ya sekondari katika moja ya shule nchini wakiwa katika vazi aina ya joho

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, amepiga marufuku matumizi ya vazi aina ya ‘Joho’ kwenye sherehe za mahafali ya ngazi za chini za elimu na kutaka litumike kuanzia ngazi ya Shahada ili kulipa heshima vazi hilo.

Waziri Ndalichako ameyasema hayo jana jijini Mbeya wakati alipokuwa anawatunuku vyeti wahitimu wa mafunzo ya uongozi na usimamizi wa elimu kwa njia ya masafa, iliyotolewa na wakala wa usimamizi na uongozi wa elimu nchini (Adem).

Amesema kuwa katika kipindi hiki ambacho serikali inafanya jitihada za kuboresha sekta ya elimu ili kuendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia ni lazima kutofautisha ngazi za elimu ili mwanafunzi wa ngazi ya chini atamani kufika ngazi ya juu.
Waziri wa Elimu, Prof Joyce Ndalichako

Amesema kuwa kwa sasa vazi hilo linaonekana kuwa ni la kawaida kwa kuvaliwa na wanafunzi mpaka wa darasa la awali hali ambayo alisema kuwa haitakiwi kuendelea na badala yake livaliwe na wanafunzi wa kuanzia ngazi ya shahada na kuendelea.

Kwenye sherehe hizo, jumla ya wahitimu 860 wa mafunzo hayo wametunukiwa vyeti na Waziri Ndalichako, ambapo amewataka kutumia taaluma waliyoipata katika mafunzo hayo ili kuinua elimu nchini.

Post a Comment

 
Top