Taarifa zinasema kwamba Uingereza itakuwa na fursa nzuri kuuona mwezi
huo siku ya Jumatatu jioni,licha ya kuwa utakaribia dunia mwendo wa saa
tano na dakika 21 muda wa GMT ambapo utakuwa umbali wa kilomita 356,509.
Wachunguzi watauona mwezi huo kuwa mkubwa zaidi kwa asilimia 7
ukilinganishwa na mwezi wa kawaida na kung'aa zaidi ya asilimia 15,
licha ya kwamba macho ya binaadamu yanaweza kupambanua tofauti hiyo.
Huku mwezi huo ukitarajiwa kutokaribia dunia hadi tarehe 25 mwezi
Novemva 2034, idara ya maswala ya hewa nchini Uingereza imesema kuwa
kutakuwa na mawingu mazito wakati mwezi huo utakapokaribia.
Huku mwezi ukizunguka dunia,kuna tofauti ya mwangaza unaotolewa na
jua.Ni wakati huo ambapo mwezi wote humulikwa na mwangaza huo na kutoa
mwezi mkubwa zaidi.

















Post a Comment