0

Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri Manispaa ya Lindi Baptista Kihanza akiwa  na viongozi  Mtandao wa Wanawake Viziwi Tanzania (MWAVITA)  


WALEMAVU Wasiosikia wako hatarini kupoteza maisha au kukosa haki za msingi kutokana watoa huduma wa  sekta ya Afya, Mahakama pamoja na Jeshi la polis kutojua jinsi ya kuwasiliana nao wakati wakihitaji.

Hali ambayo inaleta wasiwasi kwa kuhatarisha maisha yao wakati wakiwa wanahitaji na kushindwa kutatuliwa matatizo yao kwa wakati ule unaotakiwa
.
Hayo yamebainishwa na mratibu wa Mtandao wa Wanawake Viziwi Tanzania (MWAVITA) Saraha Kadila wakati alipokuwa akizungumza na watoa wa huduma wa sekta ya afya kwenye mafunzo ya siku tano inayowashirikisha waganga wafawidhi kutoka vituo vya afya, zahanati na Rufaa jana mjini hapa kwa kufadhiriwa na shirika lisilo la kiserikali la civil the foundation Society.

 Alisema wako hatarini kukosa huduma ya afya kutokana hakuna mawasiliano ya kutosha baina ya daktari, au muuguzi na kusababisha kukosa, hiyo kwa wakati unaotakiwa.
Alisema kwamba kwa hiyo ni muhimu watoa huduma wa sekta ya afya kupatiwa elimu ya jinsi ya kuwasiliana na walemavu hao,
Alitoa mfano kuna mlemavu mmoja aliuwawa na majambazi aliambiwa akae chini yeye hafahamu alionekana alikataa amri alipigwa risasi na kuwawa.
Kadila alisema kwamba hali hiyo inasambamba wanapokuwa kwenye vituo vya afya hawasikilizwi mara moja na badala yake wanaambiwa wake pembeni hali nayo ilimsababishia mama mjamzito kuipoteza maisha yake.
Alisema kwamba elimu hiyo inahitajika ifikishwe kwa kila mtoa huduma wa sekta ya afya, Mahakama, Polis na kwingineko.
Naye kaimu mkurugenzi wa Halmashauri Manispaa ya Lindi Baptista Kihanza aliwapa ushauri watoa huduma kwa sekta ya afya kujipanga kuweza kutoa huduma sahihi kwa walemavu hao ambao wako hatarishi kwa kuokoa,
Alisema kwamba mafunzo hayo ya siku tano wayazingatie kwa kufahamu alama zao kama ndiyo ishara ya kuzyngumza ili wakati wakihitaji huduma ya afya wapatiwe kwa wakati ule unaotakiwa


Post a Comment

 
Top