Wakati Serikali imewasilisha bungeni sura ya bajeti ya 2017/18
inayoonyesha matumizi ya Sh32.9 trilioni, wananchi watatakiwa kufunga
mkanda zaidi baada ya kutajwa mambo 14 yatakayowekewa nguvu kubana
matumizi kwa mwaka ujao wa fedha.
Sura hiyo ya bajeti ijayo inaonyesha ongezeko la Sh3.4 trilioni
ikilinganishwa na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/17 ya Sh29.5 trilioni
iliyosomwa bungeni Juni ambapo asilimia 40 ya bajeti hiyo, ilielekezwa
kwenye miradi ya maendeleo.
Bajeti inayotekelezwa sasa ilipunguza mambo mengi yasiyo ya lazima
ikiwamo safari za viongozi za nje ya nchi, semina na kuna wakati Rais
John Magufuli alifuta baadhi ya sherehe za kitaifa kwa lengo la kuokoa
fedha kwa ajili ya shughuli nyingine za maendeleo.
Jana, wakati Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akiwasilisha
mpango huo aliongeza maumivu 14 kutokana na uamuzi wa Serikali kuendelea
kubana matumizi yasiyo ya lazima kwa mwaka ujao.
Post a Comment