Hatimaye Chadema imenyakua kiti cha umeya wa Halmashauri ya Manispaa ya
Ubungo katika uchaguzi ambao kura za madiwani wa chama hicho zilizidi
idadi yao.
Uchaguzi huo umemfanya diwani wa Kata ya Ubungo, Boniface Jacob, aweke
historia ya kuwa mtu wa kwanza kushika umeya wa halmashauri mbili ndani
ya mwaka mmoja baada ya kupata kura 16 dhidi ya mbili za mgombea wa CCM.
Wajumbe waliotakiwa kupiga kura ni 22, lakini jana walikuwapo 18; kati
yao 15 wa Chadema na watatu wa CCM. Idadi hiyo ya kura za Jacob, ambaye
awali alikuwa meya wa Kinondoni kabla ya halmashauri hiyo kugawanywa,
inaonyesha uwezekano wa CCM kumpigia kura.
Katika chaguzi zote zilizopita, madiwani wa upinzani wamekuwa na msimamo
mkali wa kuwapa kura zote wagombea wao, jambo linaloweka uwezekano kuwa
diwani mmoja wa CCM alimpigia kura Jacob kati ya madiwani watatu
walioshiriki uchaguzi huo.
Post a Comment