0

MWENYEKITI wa Bodi ya Taifa ya Parole, Augustino Mrema amemwomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuliamuru Jeshi la Magereza liruhusu kupunguza msongamano wa wafungwa katika magereza kwa mujibu wa sheria za nchi, pamoja na kuachia wafungwa waliolipiwa faini.

Aidha, ametaka viongozi wa Magereza au wa serikali waliokwamisha wafungwa waliotimiza masharti yote wasiachiliwe kwa makusudi, wachukuliwe hatua za kinidhamu.

Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari – Maelezo, jijini Dar es Salaam ambako alitoa kilio chake dhidi ya Magereza kwamba wanakwamisha kazi ya kupunguza msongamano wa wafungwa.

Katika barua aliyoiandika kwenda kwa Waziri Mkuu, ameeleza kuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma alisema kwa sasa magereza yaliyopo katika mkoa huo kuna wafungwa 30 ambao mchakato wake umekwama kukamilika kutokana na ukosefu wa fedha.

Post a Comment

 
Top