0

Mmea hatari wazua hofu jijini Arusha
Mmea mmoja unaohatarisha maisha wa wakazi wa mji wa Arusha nchini Tanzania umeripotiwa kumea kando kando ya barabara,mashambani na kadhalika .
 
Aina mpya ya mmea usiojulikana unasemekana kumea na kuenea unaosababisha maradhi hasa ya saratani kwa mtu yeyote anayegusa .
Wanasayansi wa Taasisi ya Utafiti ya (TPRI),Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI)  na taasisi ya elimu kuhusu njaa ECHO wanafanya utafiti wa pamoja kuhusu mmea huo wa kiajabu kwa jina la 'Parthenium'.
Taarifa zaidi zafahamisha kuwa mtu anapogusa mmea huo huanza kuwa na vipele mwilini.
Aidha utafiti zaidi umeonyesha kuwa mtu anapopumua na kupata harufu ya mmea huo husababisha matatizo ya kupumua,na kudaiwa kuharibu mapafu na kusababisha saratani  mwishowe kusababisha kifo .
Kwa sasa mmea huo unamea Arusha ingawaje wanasayansi wanasema kuwa pia unaweza kumea maeneo ya nyanda za juu za Kusini,maeneo karibu na mlima Kilimanjaro na pia mikoa ya pwani.
Source: trtswahili

Post a Comment

 
Top