0
Mkuu wa mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi akizungumza na wananchi wilayani Liwale (picha na Liwale Blog)
 
Na. Mwandishi wetu, Liwale.
UWEZO mdogo wa watendaji wa vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS), umetajwa kuchangia Uchelewashaji wa malipo ya wakulima wakorosho mkoani Lindi.
 
Hayo yalieelezwa juzi novemba 20 na mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, alipozungumza na wananchi kwa nyakati tofauti katika vijiji vya Makata na Mbaya wilayani Liwale. 

Zambi ambae aliyasema hayo kufuatia malalamiko ya wakulima wa zao hilo kucheleweshwa malipo yao, alisema miongoni mwa sababu zinazochangia  ucheweshaji malipo ni uwezo mdogo wa baadhi ya watendaji wa vyama vya msingi vilivyopo mkoani humu.

Alisema kukosekana kwa weledi wamasuala ya hesabu kunachangia kuwepo kwa kasi ndogo ya kushugulikia malipo ya wakulima hao ambao wanalalamika kucheleweshewa. Kutokana na hali hiyo amewashauri wanachama wa vyama vya msingi kuwachagua watendaji wenye uwezo na waadilifu badala ya kuchagua kutokana na sifa zisizo hitajika katika kutekeleza majukumu na wajibu wao kama watendaji wa vyama hivyo.
 
"Msiwachague watendaji kwa uswahiba, chagueni walau wanaoweza kufundishika. Nikweli mfumo wa malipo ya korosho katika msimu huu ni mpya na unachangamoto, lakini uwezo mdogo wa baadhi ya watendaji unachangia ucheleweshaji unaolalamikiwa," alisema.

Mbali na agizo hilo, mkuu huyo wa mkoa amewataka wakurugenzi watendaji kuhakikisha wataalamu wa idara za ujenzi za halmashauri zao wanasimamia kwa karibu miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye halmashauri hizo.

Zambi alitoa agizo hilo baada ya kubaini baadhi ya majengo ya taasisi za umma yamejengwa chini ya viwango, nakusababisha yaanze kuharibika muda mfupi baada ya kukabidhiwa, na mengine yakiwabado yanaendelea kujengwa.

Alisema hali hiyo inawakatisha tamaa wananchi, kwasababu baadhi ya miradi wameibua na kuchangia gharama za ujenzi wake.

Huku akitoa wito wakurugenzi hao kutembelea maeneo yanayotekelezwa miradi ili kujionea utekelezaji wa miradi hiyo badala ya kukaa ofisini nakusubiri kuletewa taarifa.

Post a Comment

 
Top