0
Rais mteule wa Marekani Donald Trump alimshinda Hillary Clinton kwa kura chache katika jimbo la WisconsinRais mteule wa Marekani Donald Trump alimshinda Hillary Clinton kwa kura chache katika jimbo la Wisconsin
Aliyekuwa mgombea wa urais katika uchaguzi wa Marekani huenda akafaulu katika harakati zake za kutaka kura kuhesabiwa upya.
Donald Trump alimshinda Hillary Clinton kwa uchache wa kura katika jimbo la Wisconsin,lakini wataalam wawili wa kupiga kura wanasema kuwa matokeo hayo yanapaswa kuangaziwa kwa karibu.
Mgombea wa chama cha Green Party Jill Stein anasema kuwa amekusanya fedha za kutosha kufadhili shughuli za kuhesabu upya kura za jimbo la Wisconsin.
Hakuna ishara kwamba ushindi wa Trump ulitokana na uhalifu wa mtandaoni ,mmoja ya wataalam hao alisema siku ya Jumatano.
Mpiga kura katika jimbo la Wisconsin Mpiga kura katika jimbo la Wisconsin
Afisa mmoja wa uchaguzi katika jimbo hilo anasema kuwa wanajiandaa kwa uwezekano wa shughuli ya kuhesabu upya kura za eneo hilo.
Siku ya Jumanne,jarida la New York liliripoti kwamba kundi la wataalam ,likiongozwa na wakili wa haki za kupiga kura John Bonifaz na J Alex Halderman,mkurugenzi wa chuo kikuu cha kituo cha usalama wa kompyuta na jamii Michigan aliwasiliana na kundi la kampeni la bi Clinton.
Wataalam hao waliambia kampeni yake kuomba kuhesabiwa upya kura katika majimbo mawili ambayo alishindwa kidogo na bw Trump-Wisconsin na Pennsylvania- pamoja na Michigan ambapo alipata uongozi mdogo.

Post a Comment

 
Top