Mapema mwezi huu kiungo wa
kimataifa wa Ujerumani anayeichezea Man United Bastian Schweinsteiger
alirudi katika kikosi cha Man United baada ya kufanya mazoezi binafsi na
timu B kwa zaidi ya mwezi, licha ya Bastian kurudi kufanya mazoezi na
kikosi cha kwanza cha Man United .
Kurejea kwa Bastian Schweinsteiger Man
United bado hakumpi nafasi wala matumaini ya kupata nafasi kubwa ya
kucheza chini ya kocha wa kireno Jose Mourinho.
Kutokana na Bastian kuwa na mkataba na
Man United hadi 2018, mkataba ambao ungemuwezesha kuvuna euro milioni 18
katika kipindi hicho, Man United wanapanga kumlipa fidia ya euro
milioni 11 ilia waachane na Bastian anayehusishwa kuwa katika rada za
vilabu vya China na vya Ligi Kuu Marekani MLS.
Post a Comment