0

Gari la polisi likiwa kwenye uwanja wa Halmashauri ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi baada ya mashabiki wa mpira uwanjani hapa kuanzisha vurugu mara tu mwamuzi wa mpira wa mchezo huo kumaliza mpira,mchezo huo leo novemba 15 ulikuwa kati ya timu ya Likongowele fc Vs Sido fc.

 Ligi ya daraja la nne leo novemba 15 iliendelea kwa mchezo mmoja kati ya timu ya Likongowele fc dhidi Sido fc mchezo huo ulichezwa katika uwanja wa Halmashuri ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi ambapo katika mchezo huo timu ya Sido fc iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Katika mchezo huo timu ya Likongowele fc ilikuwa ya kwanza kufumania nyavu namo dakika ya 34 lililofungwa na Ima Ima katika kipindi cha kwanza na magoli ya timu ya Sido fc yakifungwa na Hasani Samira namo dakika ya 61 na goli la pili kifungwa na Masudi Mbwana katika dakika ya 69.

Baada ya mwamuzi wa mchezo huo kupiga kipenga cha kumaliza mpira majira saa 12:00 jioni mashabiki waliduawa na wakishangaa huku wakidai katika mchezo huo mpira ulikuwa umesimamasimama sana na kumfuata mwamuzi wa mchezo huo na kuanza vurugu uwanjani hapo na jeshi la polisi lilifanyikiwa kudhibiti vurugu hizo na kuondoka nao baadhi ya watu wanaodaiwa kuanzisha vurugu  hizo


BAADA YA KUMALIZIKA KWA MCHEZO HUO HALI IKAWA HIVI UWANJANI HAPO


Mashabikiwa mpira wakipalimia ukuta mara baada ya goli la polisi kuingia uwanjani hapo na kuanza kurusha mawe

            Baadhi ya mashabiki wakiwa kwenye goli la polisi 
              Baada ya gali la polisi kuondoka hali ilikuwa hivi uwanjani wa halmashauri

Post a Comment

 
Top