Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamadi Massauni akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika mkutano watano wa Bunge la 11 linaloebdelea Mjini Dodoma Novemba 7, 2016.
Jumla
ya askari 152 wamefukuzwa kazi mwaka huu na Jeshi la Polisi kwa sababu
ya kukiuka Sheria, Taratibu na Kanuni ya Jeshi hilo kama zilivyoainishwa
katika Kanuni za Kudumu za Polisi (PGO) namba 103.
Idadi
ya askari hao waliofukuzwa kazi imetolewa leo mjini Dodoma na Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alipokuwa
akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Maryam Msabaha aliyehitaji
kufahamu juu ya idadi ya askari waliochukuliwa hatua kwa sababu ya utovu
wa nidhamu.
Mhandisi
Masauni amesema kuwa kazi ya Vikosi vya Ulinzi na Usalama ni kulinda
raia, mali zao pamoja na mipaka ya nchi lakini kuna baadhi ya askari hao
wanakwenda kinyume na Sheria kwa kuwapiga wananchi na kuwasababishia
ulemavu pamoja na vifo hivyo Jeshi hilo limewachukulia hatua za
kinidhamu.
“Jeshi
la Polisi hufanya kazi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu
zilizopo lakini kuna baadhi ya askari wamekuwa wakikiuka maadili na
mwenendo mwema wa Jeshi letu hivyo kuanzia Januari 2015 hadi Juni 2016
tuliwachukulia hatua za kinidhamu askari 200”, alisema Mhandisi Masauni.
Naibu
Waziri huyo amefafanua kuwa baada ya askari hao kuchukuliwa hatua za
kinidhamu, walifanyiwa uchunguzi wa kina na jumla ya askari 152 kati ya
200 walikutwa na hatia hivyo hatua iliyofata ni kuwafukuza kazi.
Akizungumzia
kuhusu mpango wa Serikali juu ya kujenga nyumba za askari Polisi,
Mhandisi Masauni amesema kuwa wanatambua tatizo la makazi ya Askari
Polisi katika maeneo mbalimbali nchini hususani kwenye mikoa mipya hivyo
Serikali ina nia ya kutatua tatizo hilo kwa kuanza ujenzi wa nyumba kwa
ajili ya askari hao.
“Serikali imedhamiria kupunguza tatizo la upu
ngufu
wa makazi ya askari polisi kwa kujenga nyumba kwa awamu kupitia mpango
wa ujenzi wa nyumba 4,136 nchi nzima ambao utaanza kutekelezwa baada ya
taratibu za mkopo wa kuwezesha ujenzi huu kukamilika”, aliongeza
Mhandisi Masauni.
Post a Comment