Hatimaye Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Profesa Ndalichako amewafukuza chuo walimu waliohusika na
kumpiga mwanafunzi wa kidato cha tatu wa shule ya kutwa Mbeya.
Kwa Mujibu wa TBC- Habari za mikoani,Mpaka sasa Mkuu wa Shule na baadhi ya walimu wamefikishwa katika kituo cha polisi kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo.
Sakata hili limeibuliwa na picha ya video iliyokuwa ikisambaa katika mitandao ya kijamii.
Tayari baadhi ya viongozi wa kiserikali wamelaani tukio hilo.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala amezungumza na waandishi wa habari mkoani hapo na kuelezea mazingira halisi ya tukio hilo.
‘Tukio lilitokea Sept 26 mwalimu Frank Msigwa alitoa jaribio kwa wanafunzi lakini baadhi ya wanafunzi hawakufanya, wanafunzi walipewa adhabu ya viboko lakini Sebastian akakataa kuchapwa ndipo walimu wakamchangia kumpiga na kutoroka‘ –Amos Makala
‘Licha kwamba watuhumiwa wametoroka tangu siku ya tukio lakini nimeagiza vyombo vya sheria kuwasaka popote pale walipo, hadi sasa walimu wote wa shule hiyo akiwemo mwalimu mkuu wanashikiliwa ktk kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa maelezo‘ –Amos Makala

Post a Comment