0

Zaidi ya shilingi bilioni tatu na milionu 480 zimekusanywa katika akaunti ya kamati ya maafa Kagera huku misaada mbalimbali yenye thamani zaidi ya shilingi bilioni moja imetolewa na wasamalia wema wa ndani na je ya nchi iliyolenga kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera huku benki ya CRDB ikihamasisha jamii uchangiaji damu salama.

Tathimini hiyo imetolewa na mwenyekiti wa kamati ya maafa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu wakati alipokuwa akizungumza na ITV ofisini kwake juu ya misaada inayotolewa na wasamalia wema kutokana na athali za tetemeko la ardhi lililosababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 kujeruhiwa vibaya kati yao 434 wametibiwa na kupona huku wagonjwa sita wakiendelea na matibabu katika hospitali mbalimbali hapa nchini ambapo ameitaka jamii na wasamalia wema kuendelea kuchangia mfuko wa maafa mkoa wa Kagera kwa kuwa mahitaji ni makubwa zaidi ya fedha zilizopo.

Wito huo umeungwa mkono na benki ya CRDB tawi la Karagwe ambayo inahamasisha jamii kuchangia damu salama kwa ajili ya kuwahudumia waathirika wa tetemeko la ardhi wakati ikiadhimisha wiki ya huduma kwa wateja pamoja na kuwahudumia wazee kwa kuwapatia matibabu bure ambao wamejitokeza kwa wingi kupima afya kwa magonjwa yasiyoambukizwa.

Wakati huohuo mkuu wa wilaya ya Karagwe Bw.Godfrey Mheluka ametangaza vita dhidi ya wahalifu wanaojihusisha na mauwaji ya walemavu wa ngozi Albino na wazee kutokana na imani potofu za kishirikina wakati akihamasisha viongozi wa serikali za mita, vijiji na kata kuorozesha waathirika ambao hawajapata misaada ya chakula ili wahudumiwa kwa wakati.

Post a Comment

 
Top