Tukio la kukamtwa watu hao limetokea jana majira ya saa kumi na mbili
alfajiri katika mwalo wa Kichuguuni kijiji cha Lukumbo kata ya Butundwe
wilaya na Mkoa wa Geita, ambapo kwa mujibu wa mashuhuda, watuhumiwa hao
walikamatwa na samaki wanaodhaniwa kuvuliwa kwa sumu.
Baada ya kuhojiwa, watuhumiwa hao walikiri kufanya uvuvi haramu ndani ya
ziwa hilo, na kuwataja tu waliowatuma kutoka jijini Mwanza ambao hata
hivyo majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za uchunguzi, na kwa mujibu wa
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye ni mkuu wa wilaya ya
Geita HERMAN KAPUFI watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.
Hivi karibuni mkuu huyo wa wilaya ya Geita alifanya ziara kwenye visiwa
vinavyozunguka ziwa Victoria na kutoa elimu juu ya madhara ya uvuvi
haramu ambapo alimtaka kila mwananchi kuwa mlinzi wa mwenzake.
Post a Comment