Kikosi kazi cha ukaguzi wa miondombinu ya shirika la umeme (TANESCO)
kinachozunguka nchi nzima kusaka wateja wakubwa wanaoiba umeme kimebaini
shirika kupoteza zaidi ya sh Bilioni 1 na milioni 300 katika mikoa 19
waliyotembelea.
Kikosi hicho kinachoongozwa na na Bw John Manyama wakiwa mkoani Kagera,
wamebaini wizi wa umeme wa zaidi ya milioni 400 katika mkoa huo pekee,
na hiki ni kiwanda cha kusaga na kukoboa nafaka kilichoko Muleba Mkoani
Kagera, ambacho inaelezwa kuwa wamekuwa wakitumia umeme bila kulipa kwa
kipindi cha miaka 2 hivyo kiwanda hiki pekee kusababisha hasara ya
milioni 300.
Bw John Manyama akiongea na waandishi wa habari katika kiwanda hicho
amesema Umeme katika kiwanda hicho umekatwa, na mmiliki anahesabika
kama mwizi wa umeme.
Hata hivyo uongozi wa kiwanda hicho haukupatikana baada ya mmiliki
kudaiwa kuishi Jijini Dar Es salaam, huku anayedaiwa mkewe kugoma
kuongea na baadhi ya vibarua waliokutwa katika kiwanda hicho
wakionekana kutoelewa chochote, na kuomba kifunguliwe ili waendelee na
kazi.
Imeelezwa kuwa ukaguzi katika mikoa mingine unaendelea, na kwamba wote
waliobanika kuiba umeme wanapewa mwezi mmoja kulipia bila faini,kwamba
baada ya mwezi mmoja bila kulipa watafikishwa mahakamani.
Post a Comment