0



Kuna taarifa zinasambaa kwa kasi mtandaoni kuwa Star Tv imeuzwa.Taarifa hizi zimezua gumzo zaidi October 24,2016 baada ya mwandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania Fredrick Katulanda kuuliza swali lifuatalo...


"STAR TV IMEUZWA???
Kuna taarifa zinaeleza kuwa hali ni mbaya kwa Kampuni ya Sahara Media Group kutokana na Mkurugenzi wake Anthony Diallo kugubikwa na madeni katika benk mbalimbali ikiwemo Bank ya KCB iliyokuwa ikimdai Sh bilioni 28, deni la Mkombozi benk la malipo ya malimbikizo ya mishahara kwa wafanyakazi wake Sh bilioni 3.6 na Kodi TRA Sh bilioni 4.

Kutokana na hali hiyo imeelezwa kuwa Diallo amelazimika kuiuza Star TV kwa kampuni ya Nation Media Group wanaomiliki Magazeti ya Mwananchi, The Citizen na NTV Kenya kwa makubaliano ya kulipia madeni yake benk ya KCB na mengineyo ikiwa ni pamoja na kupunguza wafanyakazi wake zaidi ya 100.

Inadaiwa tayari ameshasaini mkataba huo"-Fredrick Katulanda.


Baada ya Mwandishi wa habari huyo kuuliza swali hilo la kuzagaa mtandaoni haya ndiyo majibu yanayodaiwa kuwa ya mmiliki wa Sahara Media Group Ltd ya Jijini Mwanza Antony Diallo ambayo pia yamezagaa mtandaoni akijibu swali aliloulizwa na Mwandishi wa Gazeti la Mtanzania Frederick Katulanda

"Tuna asset net value ya zaidi ya bil.110. Tuna mkopo kama kampuni na benki ya kcb pekee na hatuna deni kama kampuni huko mkombozi. Kuuza media company kubwa kama yetu unahitaji kibali cha tcra. Aliyeandika amemaliza kupumua! Tunapunguza wafanyakazi kutokana na uwekezaji mkubwa kwenye automation na kutegemea ununuzi wa vipindi badala ya kuvitengeneza wenyewe, ubora wa vipindi vya kutengenezwa na wengine ni bora zaidi! Aliyeandika stori ya uongo aende akalale!" Antony Diallo.


Pamoja na kuwepo kwa maelezo yanayodaiwa kuwa ni ya Antony Diallo,ifuatayo ni taarifa kutoka Sahara Media Group ambayo pia iko mtandaoni

Post a Comment

 
Top