Mgombea urais wa chama cha
Republican Marekani, Donald Trump, ameomba msamaha kwa matamshi machafu
aliyotoa kuhusu wanawake katika kanda ya video iliyozuka ya miaka 11
iliopita.
Katika kanda hiyo, Trump anasikika akijigamba kuhusu
kuwagusa wanawake sehemu zao za siri na kujaribi kushiriki ngono nao,
anasema: 'unaweza kufanya chochote unapokuwa nyota'.
Maafisa
wakuu wa chama cha Republican wameshutumu vikali matamshi yake akiwemo
spika wa bunge, Paul Ryan, aliyesema amechafuzwa roho na matamshi hayo.
Mhariri wa BBC wa eneo la Amerika kaskazini anasema hiki ni kiwango cha mzozo katika azma ya Trump kuwania urais wa Marekani
Katika
kanda iliyorekodiwa Trump aliomba radhi kwa kuonekana akisoma , na
ameahidi kuwa mwanamume bora zaidi lakini amemshutumu Bill Clinton kwa
kuwanyanyasa wanawake kingono.
Amemshutumu Hillary Clinton pia kwa kuwakandamiza na kuwaibisha waathiriwa wa unyanyasaji uliotekelezwa na mumewe.
Post a Comment