Dolnald Trump
Viongozi wandamizi wa chama cha Republican nchini Marekani
wamelaani matamshi yaliyotolewa na mgombea urais wa nchi hiyo kupitia
chama hicho Dolnald Trump aliyoyatoa mwaka 2005 yakimdhalilisha
mwanamke.
Katika mkanda huo wa video uliotolewa na gazeti la Washington Post,
Trump anasikika akimwambia mtangazaji wa kipindi kuwa unaweza kufanya
jambo lolote kwa mwanamke ukiwa nyota.
Trump ameomba radhi katika taarifa aliyoitoa kupitia video mapema
leo,lakini wakati huo huo Spika wa Bunge la Congress ambaye alikuwa
afanye kampeni na Trump baadae leo amejitoa na hatahudhuria mkutano huo
ambao ungefanyika katika jimbo la Spika Ryan huko huko Wisconsin.

Post a Comment