0

 Mchezaji wa timu ya Nangando fc (mwenye jezi ya punda kushoto)akimiliki mpira


Matokeo ya mchezo wa leo octoba 28 katika Ligi daraja la nne kulikuwa na mchezo kati ya Nangando fc dhidi ya Likongowele fc na matokeo timu ya Likongowele fc imeibuka na pointi 3 baada ya kuifunga Nangando fc magoli 3 kwa 2 katika uwanja wa halmashauri ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Katika kipindi cha kwanza timu ya Nangando fc iliweza kuongoza magoli 2 yote yakifungwa na Yuber Mmocha namo dakika ya 16 na 41 na timu ya Likongowele fc ikipata goli lililofungwa na Shafii Halfani dakika ya 31.

Kipindi cha pili Likongowele fc ilisawazisha goli dakika ya 73 liliofungwa na Ababukari Makati baada kufungwa goli hilo kocha wa timu ya Nangando fc,Selemani Nangomwa aliama benchi na kumfuata kibendela kumlalamikia ndipo mwamuzi wa mchezo huo alimpa kadi nyekundi na kutoka nje ya uwanja hali iliyopelekea wachezaji wake kukosa mwalimu wa kuwaongoza na dakika ya 86 likongowele fc ilipata goli la tatu lililofungwa na Halfani Mnyole.

Post a Comment

 
Top