0



Mchezaji wa timu ya Nangando fc (kushoto) akimpiga chenga mchezaji wa timu ya Polisi fc kwenye mchezo wa leo octoba 31 uliopigwa katika uwanja wa halmshauri ya wilaya ya Liwale.
Matokeo ya ligi daraja la nne (KUCHAUKA CUP 2016) mchezo wa leo octoba 31 kati ya timu ya Polisi fc dhidi ya Nangando fc,timu ya Polisi fc imeweza kuibuka na ushindi wa magoli 5 kwa 2 mchezo uliochezwa uwanja wa Halmashauri ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Magoli ya timu ya Polisi fc yalifungwa na David John dakika ya 13,Lawrence Fusi dakika ya 25 na 33,Yasini Nganyaga dakika ya 41 na goli la 5 lilipachikwa na Mohamed Hamed dakika ya 90.

Magoli mawili zote ya timu ya Nangando fc yalifungwa na Salumu Nombole katika dakika ya 69 na dakika ya 72 na mchezo unakamilika mpaka kipenga kinapulizwa matokeo Polisi fc 5-2 Nangando fc.

Novemba mosi kutakuwa na mchezo mmoja kati ya timu ya ABC (Mpengele) fc dhidi ya Sido fc mchezo unaotabiliwa kuwa mzuri na utakaopigwa katika uwanja wa halmashauri ya wilaya ya Liwale.




LEO NAKULETEA NJIA RAHISI SANA YA KUPATA PESA KUPITIA MITANDAO UNACHOTAKIWA SASA BOFYA >>HAPA KISHA UTAJAZA FOMUYA KUJIUNGA

KUSOMA HABARI KUHUSU BEI YA MNADA KWA MARA YA KWANZA BOFYA >>HAPA

AUDIO WAKITANGAZA BEI YA MNADA WA KOROSHO LIWALE NA NACHINGWEA

Post a Comment

 
Top