0
 
 Mchezaji wa polisi akimiliki mpira uwanjani jana kwenye mchezo wao dhidi ya Likongowele fc
 Mchezaji wa timu ya polisi fc akitolewa nje mara baada ya kuumia uwanjani
Matokeo ya mchezo wa jana octoba 25 ligi daraja ya nne (Kuchauka cup 2016) timu ya Polisi fc iliibuka na ushindi wa magoli 4 kwa 1 dhidi ya Likongowele fc mchezo uliotimua vumbi uwanja wa halmshauri ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
 
 Magoli ya timu ya  Polisi fc yalipachikwa nyavuni na Mohamed Hamed namo dakika ya 21,William Muhanga dakika ya 62,Lawrence Fusi dakika ya 89 na Yasini Nganyaga dakika ya 90 na goli la kufutia machozi la timu ya Likongowele fc likifungwa na Halfani Mnyole katika dakika ya 90. 
 
Kocha wa timu ya polisi fc,Josephfat Muhume  akizungumza na Liwale Blog alisema anashukuru kwa kupata point 3 muhimu katika mchezo wao wa kwanza lakini aliwalalamikia waamuzi wa mchezo kufuata sheria huku akiitaka uongozi wa soka wilaya kuondoa baadhi ya kasoro zinazokurekebishika ili kuboresha kiwango cha mpira.
 
Nae kocha wa timu ya Likongowele fc,Mahela Mahela alisema mamekubali kupoteza mchezo huo dhidi ya polisi fc alibainisha kilichopekea kupoteza mchezo huo ni kukosa sapoti katika kufanya maandalizi hivyo amewaomba wadau kujitokezakuweza kuiunga mkono timu hiyo.
Leo Octoba 26 kutakuwa na mchezo kati ya timu ya Black stars vs ABC (MPENGELE) fc mchezo utakaochezwa majira ya saa 10 jioni katika uwanja wa halmashauri ya wilaya ya Liwale.

Post a Comment

 
Top