kutoka nchini Misri
kuhusu Mwanamke mnene kuliko wote duniani ambaye anatajwa kufikisha
uzito wa kilo 500.
Kwa mujibu wa jarida la Daily Mail, inaelezwa kuwa mwanamke huyo
aitwaye Iman Ahmad Abdulati mwenye miaka 36 hajawahi kutoka ndani kwa
miaka 25 na amekua akiongezeka uzito wake kwa haraka mpaka kufikia kilo
500 zinazompa shida ya kujifanyia usafi na hata kula. Ripoti ya
madaktari inaonesha kuwa mwanamke huyu anasumbuliwa na maambukizi ya
bakteria wanaoshambulia ukuaji wa mwili.
Akiwa na miaka 11 alianza kusumbuliwa na tatizo hilo ingawa wazazi
wake wanakiri kuwa hawakudhani kuwa ni tatizo lakini siku zilivyozidi
kwenda ndipo wakabaini kuwa halikua jambo la kawaida hivyo wakaamua
kutafuta wataalamu ambao walitoa ripoti kuwa ana matatizo ya mwili wake
kukaa na maji mengi bila kuyatoa nje kitu ambacho sio cha kawaida kwa
binadamu.
Post a Comment