0

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), Stanslaus Kadugazile (Kushoto) akihojiwa na waandishi wa habari. 
Dar es Salaam. Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), imekubaliana na Wizara ya Elimu kupitia upya mchakato wa mgawo uliofanyika kwa mara ya kwanza ili kuondoa kasoro zilizojitokeza  awali.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Stanslaus Kadugazile amesema makubaliano hayo yamefikiwa baada ya kukutana leo (Alhamisi) na viongozi wa wizara hiyo pamoja na wahusika wanaopokea, kupanga na kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
“Tumejadiliana juu ya changamoto zote zilizojitokeza kwenye mgawo uliokwenda vyuoni ikiwa ni pamoja na viwango vidogo vya fedha walizopangiwa wanafunzi kwa ajili ya chakula na malazi, Vitabu na viandikwa pamoja na ada na kuona ipo haja ya kufanya marekebisho ya viwango hivyo vilivyopangwa kwa wanafunzi haoili kuweza kukidhi mahitaji halisi kwa kila mwanafunzi anayestahili kupata mkopo na kutoa mgawo vipya tofauti na ya kwanza,”amesema.

Post a Comment

 
Top