Mashindano ya mpira wa miguu ligi
daraja la nne maarufu (Kuchauka cup 2016) katika wilaya ya
Liwale mkoani Lindi inatarajia kutimua vumbi octoba 24 mwaka huu,ligi hiyo ikiwa na jumla ya timu 7 tayari
zimethibitisha kushiriki.
Kwa mujibu wa katibu mkuu wa
chama cha mpira wa miguu wilaya ya Liwale (Lidifa),Nourdin Kazumari amesema
timu 7 zilizothibisha kushiriki michuano hiyo ni timu ya New generation
fc,Nangando fc,Polisi fc,Likongowele fc,Black stars,ABC (Mpengere) fc na Sido
fc.
Timu pekee ya ABC FC ndio inayoshiriki
mashindano haya kutoka nje ya mjini huku timu zingine zikikataa kushiriki
mashindano zikidai mashindano mengi yanayoendeshwa wilayani timu za mjini
zinapendelewa hata kama timu inayotoka nje ya mjini ikiwa na kiwango.
Mchezo wa ufunguzi Katika
michuano hiyo inayotarajia kuanza kutimua vumbi jumatatu octoba 24 kati ya timu
ya New generation dhidi ya Nangando fc mchezo utakaochezwa uwanja wa
halmashauri ya wilaya ya Liwale.
Mchezo wa pili utachezwa siku ya
jumanne octoba 25 kwa kuzikutanisha timu ya maafisa wa polisi wilayani hapa
Polisi fc dhidi ya Likongowele fc,octoba 26 kutakuwa na mchezo kati ya Black
Stars dhidi ya ABC (Mpengere) FC,octoba 27 kutakuwa na mchezo kati ya Sido fc
dhidi ya New generation na octoba 28 kutakuwa na kati ya Nangando fc na
Likongowele fc.
Octoba 31 kutakuwa na mchezo kati
ya Polisi fc dhidi ya Nangando fc,novemba mosi kutakuwa na mchezo kati ya ABC
FC dhidi ya Sido fc,novemba 2 mchezo kati ya timu ya Black Stars dhidi ya New
generation,novemba 3 mchezo kati ya timu ya Polisi fc dhidi ya Sido fc na
novemba 4 kutakuwa na mchezo kat ya timu ya Likongowele fc dhidi ya ABC FC
07/11/2016 BLACK STARS Vs SIDO FC
08/11/2016 NEW GENERATION Vs POLISI FC
09/11/2016 NANGANDO FC Vs ABC (MPENGERE) FC
10/11/2016 BLACK STARS FC Vs LIKONGOWELE FC
11/11/2016 SIDO FC Vs NANGANDO FC
14/11/2016 POLISI FC
Vs BLACK STARS FC
15/11/2016 LIKONGOWELE
FC Vs SIDO FC
16/11/2016 ABC
(MPENGERE) FC Vs NEW GENERATION FC
17/11/2016 NANGANDO FC
Vs BLACK STARS FC
18/11/2016 NEW
GENERATION FC Vs LIKONGOWELE FC
21/11/2016 POLISI FC Vs ABC (MPENGERE) FC
Post a Comment