Makachero katika Uwanja wa ndege wamemtia Mbaroni mwanamke Raia wa Brazil akiwa na Dawa za Kulevya
Makachero katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julias Mwalimu nyerere
wamemtia Mbaroni mwanamke Lilian Jesus Fortes mwenye umri wa miaka 32
Raia wa Brazil ambaye baada ya kupekuliwa alikutwa na Dawa za Kulevya
aina ya Cocaine kilo 2 na Robo ambazo aliziweka katika begi.
Kamanda wa Polisi kikosi cha Uwanja wa Ndege Martin Otieno akizungumza
na Chanel amesema Mwanamke huyo alikuwa ameshuka katika ndege ya Etihad
akitokea Katika mji wa Sao Paul nchini Brazil na baadae kupitia Abu
dhabi ambapo alifika katika uwanja wa ndege wa kimataifa kwa ajili ya
kuunganisha safari na shirika la ndege la Ethiopia kuelekea nchini
Malawi.
Amesema Mtuhumiwa huyo alikuwa amezifunga na kuhifadhi katika pakiti za
Aluminium ambapo na kushonea Vizuri katika begi huku pembeni akiweka
vitabu ili zisibainike katika mashine maalum za Ukaguzi.
Kamanda Otieno ameeendelea kuwaonya watu wote wanaotumia uwanja huo
kupitisha dawa za kulevya au nyara zozote za Serikali kuwa wamejipanga
na wale watakaojaribu watakumbana na Mkono wa sheria.
Post a Comment