0

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman

Wanasheria wabobezi wa masuala ya haki na uhalifu wa kimataifa kutoka nchi mbalimbali duniani wamekutana jijini Arusha kutafuta ufumbuzi na kuboresha uhusiano kati ya nchi za Afrika na Mahakama ya ICC pamoja na taasisi zinazohusu haki na amani
Akizungumza mara baada ya kufungua mkutano huo Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande, amesema migongano iliyopo kati ya nchini nyingi za kiafrika na Mahakama ya ICC, ni ya kimtazamo zaidi.

Jaji Chande ameongeza kuwa mkutano huo una umuhimu mkubwa wa kutengeneza njia zitakazoleta mawazo chanya ya kutatua matatizo ya nchi hizo bila kuvunja misingi ya haki na amani ya nchi husika.

Jaji Mkuu amesema kuwa nchi nyingi za kiafrika ziliomba viongozi wa Afrika wasipelekwe mahakamani katika kipindi chao cha uongozi huku mkataba wa mahakama hiyo ukiwa hautambui kinga hiyo jambo linaloleta migongano ambayo kuna umuhimu wa kuitatua.

Post a Comment

 
Top