0
Ligi Kuu soka Tanzania bara zimechezwa leo Jumatano ya October 12 2016 katika viwanja tofauti Tanzania, kwa upande wa mabingwa watetezi wa Ligi hiyo klabu ya Dar es Salaam Young Africans wameshuka dimbani kucheza mchezo wao wa 7 wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Mtibwa Sugar uwanja wa Uhuru.
Yanga ambao wamekuwa na rekodi ya ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar katika kipindi cha misimu miwili, wameendeleza rekodi yao kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-1, magoli ambayo yalifungwa na Obrey Chirwa dakika ya 45, Simon Msuva dakika ya 68 na Donald Ngoma akitokea benchi dakika ya 80 wakati goli la Mtibwa lilifungwa na Haruna Chanongo dakika ya 64.
Mara ya mwisho Mtibwa Sugar na Yanga kucheza ilikuwa ni October 6 2016 uwanja wa Taifa Dar es Salaam, siku ambayo Mtibwa walijaribu kutaka kuondoa uteja ila ikashindikana na kuishia kuambulia suluhu ya 0-0, Yanga ambao wanaonekana kama kupungua kasi kwa mechi zao za karibuni, watakuwa na mtihani Jumapili dhidi ya Azam FC katika uwanja wa Uhuru pia.

 Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizochezwa leo October 12 2016
 
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizochezwa leo October 12 2016
  • Mbeya City 0-2 Simba
  • Mbao FC 3-1 Toto Africans
  • Mwadui FC  2-0 African Lyon
  • Majimaji FC 0-1 Kagera Sugar
  • JKT Ruvu 0-0 Prisons
  • Stand United 1-0 Azam FC

Post a Comment

 
Top