Kapteni wa timu ya Sido fc akipewa zawadi baada ya kushika nafasi ya pili ligi ya Nangando under 17 cup leo octoba 2
Diwani wa kata ya Nangando,ndugu Jafari Mkungu akimkabidhi mbuzi kapteni wa timu ya Makonji fc (The Heroes fc) na madhumuni ya mashindano haya ilikuwa kuendeleza vipaji vya wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 17 .
Timu ya Makonji fc (the heroes fc) yatawazwa
mabingwa wapya Ligi ya Nangando under 17 cup baada ya kuifunga timu ya Sido
fc Magoli magoli 4 kwa 2 mchezo
uliopigwa uwanja wa shule ya msingi Muungano wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
Katika mchezo huo wa
fainali kati ya timu ya Sido fc dhidi Makonji fc (The heroes fc) katika kipindi
cha kwanza mpaka dakika 45 za mapumziko walitoka sare ya magoli 2 kwa 2
Kipindi cha pili timu
ya Makonji fc iliongeza magoli 2 mpaka dakika 90 zinakamilika matokeo yalikuwa Makonji fc (the heroes fc) 4-2 Sido fc
magoli ya makonji fc yalifungwa na Haidari Mohamedi,muksini Ndumbi,Haidari Mohamedi na Saidi matuli pia Magoli ya Soido fc yalifungwa na mchezaji mmoja Ikram Kigwalilo
MSHINDI WA KWANZA KATIKA MASHINDANO HAYO AMEPATA MBUZI NA MASHINDI WA PILI SIDO FC IMEPATA SH. 15000/=
Post a Comment