Timu ya Majimaji ya Songea imeendelea kuwa shamba la bibi kwa kugawa
point baada ya leo kupigwa mabao 2-0 na Stand United katika uwanja wake
wa nyumbani wa Majimaji mjini Songea.
Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara umeifanya Majimaji kupoteza mchezo wa 7 mfululizo huku ikiwa haina point hata moja, na hivyo kuendelea kushika mkia katika msimamo wa ligi hiyo.
Mchezo huu ni kwanza kwa kocha Kally Ongala ambaye alirejeshwa kuinoa klabu hiyo baada ya kuona mwenendo wake ukiwa wa kusuasua.
Matokeo hayo yanaifanya Stand United kuzidi kujiimarisha zaidi katika msimamo wa ligi kuu ikifikisha point 15 nyuma ya vinara Simba yenye point 17, na kulinda rekodi yake ya kutopoteza mchezo wowote kati ya michezo saba tangu kuanza kwa ligi.
Katika mechi nyingine, Mbao FC imelazimishwa suluhu ya 0-0 na JKT Ruvu katika dimba la CCM Kirumba, huku Mtibwa Sugar ikiichapa African Lyon bao 1-0 katika dimba la Manungu, Morogoro.
Mbeya City imeifunga Mwadui FC bao 1-0 Sokoine Jijini Mbeya na Kagera Sugar imeitandika Tanzania Prisons mabao 2-0.

Post a Comment