Sakata
la watumishi hewa sasa limefikia pabaya baada ya msako wa watu
wanaolipwa fedha bila kuwapo kazini kumkumba Mbunge Makete (CCM),
Profesa Norman Sigalla ambaye alikuwa mkuu wa Wilaya ya Songea.
Wadau
walishawahi kueleza kuwa msako wa watumishi hewa uliwahusu wafanyakazi
wa kariba ya chini na hivyo kuokoa fedha kidogo, lakini sakata la
Profesa Sigalla limeonesha kuwa hata kariba ya juu serikalini inahusika.
Profesa
Sigalla anadaiwa kupokea mshahara wa ukuu wa wilaya kwa miezi mitano
baada ya kuacha kazi hiyo wakati wa Uchaguzi Mkuu na baadaye kuchaguliwa
kuwa mbunge kwa tiketi ya CCM.
Hali hiyo imeisababishia Serikali hasara ya Sh23 milioni.
Baada
ya kuacha kazi hiyo ya kuteuliwa na Rais, inadaiwa kuwa Profesa Sigalla
aliendelea kupokea mshahara wake wa ukuu wa wilaya wa Sh4.6 milioni
kutokana na ofisa utumishi wa ofisi ya katibu tawala wa Mkoa wa Ruvuma
kumrudisha kwenye orodha ya malipo ya mshahara.
chanzo:gazeti la mwananchi
Post a Comment