0

 Biashara ya Simu za kisasa maarufu kama Smartphone au Simu Janja imeendelea kukua na kuongeza ushindani wa makampuni ya utengenezaji wa bidhaa hizo duniani kote. Leo October 26, 2016 mtu wangu nimeipata hii kuhusu nchi iliyofanya vizuri kwenye biashara ya Smartphone duniani.

Ripoti iliyotolewa na kampuni ya GFK ya Ujerumani inaonesha kuwa, mpaka kufikia robo ya tatu ya mwaka huu, China imeongoza katika soko la simu za smartphone na kuendelea kukua zaidi, huku ikiongeza msukumo mkubwa wa ukuaji wa soko la simu hizo duniani.

Ripoti hiyo inasema simu milioni 353 aina ya smartphone zimeshauzwa katika robo ya tatu ya mwaka huu duniani kote, na idadi hiyo imetajwa kuongezeka kwa asilimia 7.5 kuliko mwaka 2015 kwa wakati kama huo, huku simu milioni 113 kati ya hizo zikiuzwa katika soko la China pekee.

Post a Comment

 
Top