Baada
ya chama cha NLD kutokuwa na mwenyekiti kwa miezi kadhaa sasa kufuatia
kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Emmanuel Makaidi, Kamati Kuu ya chama hicho imemteua Oscar Emmanuel Makaidi kuwa mwenyekiti wa NLD.
Oscar
Makaidi amejitangaza rasmi leo katika mkutano wa Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es
Salaam.
Amesema
kamati kuu ya NLD ilikaa kikao Aprili 27,2016 na kumteua kuwa
mwenyekiti wa chama hicho ambapo anaziba pengo lililoachwa na marehemu
baba yake.
Ukawa pia imemtangaza rasmi Oscar Makaidi kuwa mwenyekiti mwenza wa umoja huo kupitia chama cha NLD.
Post a Comment