0

Ummy Mwalimu (Kulia) akizungumza na bi. Ulla Mullar (Kushoto)

Imeelezwa kuwa asilimia 73 ya wanawake nchini Tanzania hawatumii uzazi wa mpango, ikimaanisha kuwa ni asilimia 27 pekee ndiyo wanaoumia njia mbalimbali katika kudhibiti uzazi.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo amekutana na Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango la Engenderhealth bi. Ulla Mullar.

Katika mazungumzo hayo Waziri Ummy amesema hivi sasa asilimia 27 ya wanawake wa kitanzania ndiyo wanaotumia njia za uzazi wa mpango ambapo serikali ilijiwekea malengo mwaka 2012 kwamba ifikapo mwaka 2020 ifikie asilimia 50 ya matumizi ya njia ya uzazi wa mpango.

Waziri Ummy amesema kuwa wamekubaliana kuendeleza ushirikiano katika huduma za uzazi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya upasuaji wakati wa uzazi, kukarabati wodi za wazazi na pia kutoa mafunzo kwa watumishi wa sekta ya afya katika kumuepusha mama na kifo wakati wa uzazi.

Post a Comment

 
Top