0

Jeshi la Polisi mkoani Rukwa kwa ushirikiano na kikosi cha askari wanyamapori na maafisa uhamiaji,katika operesheni maalumu ya Faru iliyofanyika wilayani Nkasi,limefanikiwa kukamata silaha 25,nyara za serikali,mitambo ya kutengenezea pombe haramu aina ya gongo, pamoja na zana zilizokuwa zikitumika kwenye uvuvi haramu katika ziwa Tanganyika.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Rukwa Kamishna Msaidizi wa polisi George Kyando,akiongea mjini Namanyere wilayani Nkasi amesema operesheni hiyo ya Faru,iliyofanyika kwa siku tisa wilayani Nkasi baada ya taarifa za kushamiri kwa uhalifu wilayani humo,ilifanikiwa pia kuwakamata wahamiaji haramu zaidi ya 200,kundi kubwa wakitokea Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo.

Baadhi ya wakazi wa mji wa Namanyere wakiongelea juu ya operesheni hiyo,wamelipongeza Jeshi la polisi kwa hatua hiyo ya kukamata silaha zinazomilikiwa kinyume cha sheria, kwani zinachangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la vitendo vya ujangili kwenye mikoa ya Rukwa na Katavi.

Source: Itv

Post a Comment

 
Top