Kamishna
wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam CP Simon Sirro akipokea hundi ya
milioni 50 kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF,
Godius Kahyarara kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi Kiluvya Gogoni.
Mkurugenzi
wa NSSF, Godius Kahyarara akizungumza na waandishi wa habari katika
makabidhiano ya hundi ya milioni 50 kwa jeshi la Polisi kwa ajili ya
ujenzi wa kituo cha Polisi Kiluvya Gogoni.
Kamishna
wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, CP Simon Sirro akizungumza na
waandishi wa habari Jijini Dar es salaam baada ya kupokea hundi ya
milioni 50 kutoka kwa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa ajili ya
ujenzi wa kituo cha Polisi Kiluvya Gogoni.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SHIRIKA
la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limechangia kiasi cha Milioni 50
kusaidia ujenzi wa kituo cha Polisi Kiluvya Gogoni ikiwa ni katika
kukabiliana na changamoto ya kukua kwa miji kwenda sambamba na ongezeko
la uhalifu.
Akizungumza
wakati wa kutoa hundi ya milioni 50, Mkurugenzi wa NSSF, Godius
Kahyarara amesema kuwa huu ni utaratibu wao katika kuisaidia jamii
katika nyanja za elimu, Afya, Mazingira, Michezo na maeneo mengine
yaliyoainishwa katika sera.
Kahyarara
amesema kuwa kutokana na polisi kupanua wigo ili kufika katika matukio
kwa haraka zaidi jeshi linahitaji kuongeza vituo maeneo mbalimbali na
NSSF imeona vyema kushiriki katika suala zima la kuhifadhi na kulinda
jamii na mali zao.
Kamishna
wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, CP Simon Sirro ameshukuru kwa
hatua iliyochukuliwa na NSSF kwa kuweza kuwasaidia katika ujenzi wa
kituo cha Kiluvya Gogoni kwani ulisimama kwa muda kutokana na ukosefu wa
hela.
Akipokea
hundi amewaomba mashirika mengine kujitokeza kusaidiana na polisi
kuweza kuwasaidia kwenye ujenzi wa vituo ili kusogeza huduma ya haraka
zaidi kwa wananchi pale matukio ya kiuhalifu yanapotokea.
Post a Comment