0


Morogoro. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa siku moja kwa uongozi wa Manispaa ya Morogoro kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo na kuyatangaza kesho.

“Mbali na kutenga maeneo pia nawaagiza muwasaidie wafanyabiashara hawa kuunda vikundi kulingana na aina ya biashara wanazozifanya ili kuwawezesha kupata mikopo kwa urahisi kutoka katika taasisi za fedha” amesema.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo alipotembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi Msamvu unaojengwa kwa ubia kati ya Manispaa ya Morogoro na Mfuko wa Pensheni wa LAPF.

Awamu ya kwanza ya mradi huo inatarajiwa kufunguliwa Agosti 12 mwaka huu utakuwa ni kituo cha mabasi cha kwanza cha kisasa Tanzania ambapo Waziri Mkuu amezitaka halmashauri zote zilizoko makao makuu ya mikoa nchini kuiga mfano huo.

Kwa upande wake Meneja wa mradi huo Stanley Mhapa alisema mradi huo umegharimu sh. bilioni 40 ambapo Manispaa inamiliki asilimia 40 ya hisa na mfuko wa LAPF unamiliki asilimia 60.

“Mafanikio ya mradi huu ni pamoja na kuiwezesha Manispaa kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka sh 350,000 kwa siku hadi kufikia sh. milioni 1.7 kwa siku,” amesema.

Post a Comment

 
Top