Afisa
Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed katikati
akimkabidhi hati yake ya kiwanja mteja wao aliyenunua kiwanja cha Kilwa,
Mubarack Kirumirah kulia. Kushoto ni Mratibu wa Masoko na Mawasiliano
wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
WATEJA wa viwanja vya Bayport Financial Services wilayani Kilwa,
mkoani Pwani wameanza kupewa hati zao kutoka mradi wa Kilwa Msakasa
unaoendeshwa na taasisi hiyo inayojihusisha na mikopo, huku ikiwa na
dhamira ya kuwakwamua wateja wao na Watanzania kwa ujumla.
Mradi wa Kilwa Msakasa ni miongoni mwa miradi kadhaa inayoendeshwa
na taasisi hiyo ikiwamo Bagamoyo, Vikuruti, Kigamboni na Kibaha na
kujikita kurahisisha pia utoaji wa hati kwa wateja wao waliokamilisha
utaratibu rahisi wa malipo ya viwanja hivyo.
Mteja
wa Bayport Financial Services, Mubarack Kirumirah kulia akitia sahihi
kabla ya kukabidhiwa hati yake ya kiwanja cha Kilwa. Anayeshuhudia ni
Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed.
Shughuri za maandiko ya kukabidhiana hati zikiendelea katika ofisi za Bayport jana.
Alisema taasisi yao imeendelea kuboresha huduma zao ili
kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anapata uwezo wa kumiliki kiwanja
chenye hati kwa ajili ya kuvitumia katika mipangilio ya maisha yao.
“Bayport ni taasisi ambayo imekusudia kuona watu wanamiliki
viwanja vyenye hati kwa urahisi, hivyo kila aliyekopa kiwanja au kununua
kwa fedha taslimu kupitia kwetu atakabidhiwa hati yake haraka
iwezekanavyo kwa sababu tumedhamiria kuwakwamua wateja wetu wote, hivyo
wale ambao hawajapata fursa ya kuhudumiwa na ofisi yetu wafanye hivyo
ili waone namna gani Bayport ipo kwa ajili yao,” alisema Mercy.
Naye Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed,
aliwataka wateja wao kutembelea katika ofisi za taasisi yao zilizoenea
nchi nzima ili wapate huduma bora za mikopo ya viwanja inayowahusu
watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi pamoja na
wajasiriamali.
“Tunajivunia kufanya kitu tofauti kwa wateja wetu ndio maana kila
anayepata kiwanja kwetu tunahakikisha kwamba hapati usumbufu wowote wa
kufuatilia hati sehemu husika badala yake sisi ndio tumechukua jukumu
hilo tukiamini kwamba jambo hili litakuwa mkombozi kwa wateja wote,”
alisema Mohamed.
Naye mteja wa Bayport aliyekabidhiwa hati yake ya kiwanja cha
Kilwa, Mubarack Kirumirah Hamidu, aliwashukuru Bayport kwa kufanya kazi
nzuri inayowaendelea usumbufu wateja wao kufuatilia hati za viwanja,
jambo linaloonyesha utofauti mkubwa katika suala zima la ardhi.
“Nashukuru kwa kupata hati ya kiwanja change kwa kipindi
kisichozidi miezi mitatu tangu nilipojitokeza kununua kiwanja cha Kilwa
Msakasa, hivyo suala hili limenifurahisha na kuwaeleza Watanzania
wenzangu kuchangamkia kununua viwanja vya Bayport,” alisema.
Wengine waliokabidhiwa hati zao za viwanja vya Kilwa ni Mrina
Harish Mawji, Jigar Patel, Amina Haidari Amani, Victoria Ambrose Kundi
na wengine wengi ambao wamekuwa miongoni mwa Watanzania waliojitokeza
kwa wingi kuchangamkia fursa ya mikopo ya viwanja vya Bayport
vinavyoendelea kutolewa na taasisi hiyo nchini Tanzania.
Post a Comment