Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Arusha Mjini kupitia
kikao chake cha Kamati ya Utendji kilichofanyika tarehe 24/09/2016
kimefanya uteuzi wa nafasi ya Katibu wa Wilaya kwa kumteua ndugu STEVEN
URASSA kuwa Katibu wa Wilaya na kuchukua nafasi iliyokuwa imeachwa wazi
na aliyekuwa Katibu wa Wilaya Ndugu Lewis Emmanuel Kopwe kwa kukoma
uongozi kwa kujiuzulu kwa hiari yake ( Ibara ya 6.3.4 (a) ) Uteuzi huu utaanza tarehe 26/09/2016 mara baada ya makabidhiano ya Ofisi kufanyika.
Kabla
ya Uteuzi huu ndugu STEVEN URASSA alikuwa Mwenyekiti wa Kata ya
Ngarenaro na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa TCA katika Kata ya
Ngarenaro.
Uteuzi
huu ni kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA Toleo la 2006 ( Kama
ilivyoboreshwa 2014 ) Ibara ya 6.3.5 Kuziba nafasi wazi za Uongozi (a)
(b) (c) Uteuzi
huu pia umezingatia KANUNI ZA UENDESHAJI KAZI ZA CHAMA SURA YA KUMI ;
10.0 MAADILI YA VIONGOZI, SIFA MAHUSUSI ZA VIONGOZI NA MAADILI YA
WANACHAMA.
Tunaomba apewe ushirikiano wote katika kutekeleza majukumu yake.
Imetolewa na;
Kitengo cha Habari na Mawasiliano
CHADEMA WILAYA YA ARUSHA MJINI
Post a Comment