Wapinzani nchini
Gabon wamechoma moto jengo la bunge la nchi hiyo baada ya Rais Ali Bongo
kutangazwa kuwa mshindi wa Uchaguzi wa Rais Uliofanyika siku ya
Jumamosi dhidi ya mpinzani wake mkuu Jean ping.
Kwa upande wake
mgombea huyo aliyeshindwa amesema pia vikosi vya usalama vimeshambulia
makao yake makuu kwenye mji mkuu Libreville.
Jean Ping aliliambia
shirika la habari la ufaransa AFP kuwa vikosi vya ulinzi vimetumia
helkopta kushambulia kwa mabomu jengo hilo kabla ya kulivamia.
Amearifu kuwa watu 19 wamejeruhiwa baadhi yao wakipata majeraha mabaya.
Awali,
polisi katika mji mkuu wa Gabon, Libreville walitumia mabomu ya kutoa
machozi kuweza kuwatawanya wafuasi wa Jean Ping, waliokuwa wamejawa na
hasira na ambao wanaamini kuwa matokeo hayo ya uchaguzi yalikuwa ya
udanganyifu.
Ni kura chache tu, zilizomuwezesha Bwana Bongo
kumshinda mpinzani wake na hatimaye kutangazwa kuwa mshindi, huku eneo
analotoka akionekana kupata kura nyingi zaidi.
Ujumbe uliokuwa
ukiwakilisha upinzani katika Tume ya Uchaguzi ulitoka nje na kukataa
kusaini karatasi, zinazompa ushindi Rais Bongo.
Mwangalizi wa
Uchaguzi huo, kutoka Jumuia ya Ulaya, Sara Crozier ameelezea hali ilivyo
katika mji mkuu wa nchi hiyo, Libreville, kuwa ni ya wasiwasi.
Familia ya Bongo imekuwa madarakani katika nchi hiyo ya Afrika ya kati kwa takriban miongo mitano
Post a Comment