0


Wanafunzi 50 wa shule za msingi na sekondari katika Wilaya ya Dodoma wamebainika kupata ujauzito katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Agosti 2016.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christina Mdeme wakati akitoa semina kwa wasimamizi wa mitihani katika manispaa ya Dodoma..

“Wanafunzi wengi wamepata mimba, na kuna baadhi ya kesi mahakamani ila kikwazo kikubwa tunakipata kutoka kwa wazazi na ndugu ambao huwaficha wanaohusika kuwapa mimba wanafunzi.

Mndeme ameongeza kuwa baadhi ya wanafunzi wakishapata mimba kutokana na kulazimishwa kutokusema ukweli, huwakana waliowapa mimba hivyo kusababisha kesi nyingi kukosa ushahidi.

Jumla ya wasimamizi wa elimu 381 wamepatiwa mafunzo na kutakiwa kuwa waaminifu katika kusimamia mitihani ya kitaifa inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Post a Comment

 
Top