0

Handeni.  Halmashauri ya Wilaya ya Handeni  mkoani Tanga, inapoteza zaidi  ya Sh 240 milioni kwa  mwaka kutokana na mawakala kushindwa kuwasilisha  kiwango  cha ushuru walichokubaliana  kukusanya katika mikataba.

Mwenyekiti  wa  Halmashauri  hiyo,  Ramadhani Dilliwa  alisema  kutokana  na kukiuka mkataba huo, ilitarajia kuanza  kukusanya ushuru huo juzi.

 Akizungumza katika  kikao cha Baraza  la Madiwani  wa Halmashauri  hiyo, Dilliwa alisema uamuzi huo utasaidia kuokoa fedha nyingi zinazopotea.

Makamu  Mwenyekiti wa Halmashauri  hiyo  ambaye  pia ni  Mwenyekiti  wa Kamati ya  Fedha, Uongozi na Mipango,  Abdallah  Pendeza  alisema  halmashauri inakabiliwa na  changamoto ya kukosa mapato kutoka  kwa  wazabuni.

Post a Comment

 
Top