0

Lushoto. Askari wa Kampuni ya Ulinzi ya Tele Security ya Tanga, ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi waliovamia Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (Sekomu) wilayani hapa usiku wa kuamkia jana.

Majambazi hao ambao idadi yao inakadiriwa kuwa kati ya 10 hadi 15, walivamia mabweni mawili waliyokuwa wakilala wanafunzi wasichana kisha kumwaga petroli katika mabweni hayo na kulipua kwa kiberiti bweni moja ambalo halikuwa na watu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba alisema tukio hilo lilitokea saa tano usiku wa kuamkia jana katika mabweni yaliyo jirani na ofisi kuu ya chuo hicho. Mlinzi aliyeuawa ni Yohana Shemzigwa (34) na mwenzake, Abuu Rajab (33) alijeruhiwa.

Post a Comment

 
Top