0

Takriban watu 29 wamekufa maji baada ya boti ya wahamiaji kuzama karibu na pwani ya Misri,kulingana na maafisa.
Boti hiyo ilikuwa imewabeba abiria 600,ambao kati yao 150 wameokolewa ,kulingana na chombo cha habari cha taifa hilo.

Kisa hicho kilitokea karibu na pwani ya Kafr al-Sheikh,maafisa wanasema.
Tukio hilo la siku ya Jumatano linajiri wakati ambapo muungano wa Ulaya umeonya kwamba wahamiaji wanaolekea Ulaya wanatumia Misri kama mwanzo wa safari yao.

Post a Comment

 
Top