SHAHIDI
wa 19 katika kesi ya utakatishaji fedha na wizi wa kutumia mfumo wa
mtandao wa kibenki wa Sh bilioni saba, inayowakabili wafanyakazi 13 wa
benki ya Exim tawi la Arusha,Thadeus Madawe (37), amesema ushahidi wa
risiti za benki waliupata kutoka kwa kampuni za utalii zilizolipa benki
kwa ajili ya kupata huduma ya utalii ndani Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro (NCAA).
Madawe
amesema mahakamani leo wakati akiongozwa kutoa ushahidi na Mwanasheria
Mwandamizi wa Serikali, Poul Kaduchi mbele ya Hakimu Mfawidhi wa
Mahakama ya Wilaya ya Arusha na Arumeru, Deusdedit Kamugisha.
Amesema,
NCAA iliomba malipo ya risiti za benki kwa kampuni hizo za kitalii
baada ya kubaini kuwa karatasi ya kuonesha kuweka na kutoa fedha benki
ya Mamlaka hiyo, akaunti ya dola ya shirika hilo na kitabu cha mizania
ya malipo zinatofautiana na bila ya kupata karatasi ya kuweka fedha hizo
wasingeweza kubaini wizi huo.
Madae
amesema, kampuni za kitalii zilitoa ushirikiano na ziliwasilisha baadhi
ya karatasi za kuweka fedha kwa uongozi wa NCAA na walipofanya
uchunguzi ndipo walipobaini baadhi ya dola 790,000 hazikuingia katika
akaunti ya shirika hilo.
Amesema
hayo yote yalifanyika kwa kushirikiana na jeshi la polisi Arusha na
makao makuu Dar es Salaam na timu yake ya uchunguzi na nyaraka zote
kukabidhi polisi katika ofisi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO).
Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo na shahidi wa 21 katika kesi
hiyo atatoa ushahidi wake.
Watuhumiwa
hao kwa nyakati tofauti kati ya mwaka 2011 hadi 2012, walifanikisha
wizi huo kwa kuziibia kampuni mbalimbali za utalii na mamlaka ya hifadhi
ya Ngorongoro kupitia kugushi nyaraka za akaunti ya dola na fedha za
kitanzania na mfumo wa malipo ya kadi.
Mshitakiwa
wa kwanza katika kesi hiyo ni Bimal Gondalia Gomes (34) ambaye alikuwa
Meneja wa Exim, tawi la Arusha, Lilian Mgaya (33), Livistone
Mwakiyaba(36),Joyce Kimaro (36), Daud Mosha.
Wengine
ni Doroth Tigana (50),Evans Kashebo(40), Tuntufe Agrey (32),Joseph
Meck(34) ,Janes Massawe (32), Christophe Lyimo(34), Gervas Lubuva ambaye
si mfanyakazi wa benki ya Exim na Deodet Chacha (35).
|
Post a Comment