0


Baadhi ya wafanyabiashara wakishiriki zoezi la usafi kikamili leo jumamosi septemba 10
Mkuu wa wilaya akizungumza na wafanya biashara katika soko kuu la Liwale leo mara baada ya kushiriki zoezi la usafi katika soko hilo na kutoa nafasi ya watu kuweza kutoa maoni yao.

Wafanyabiashara wa wilaya Liwale mkoani Lindi katika  soko kuu la Liwale mjini leo asubuhi baada ya kufanya ushafi wa kila jumamosi na mkuu wa mkuu wa wilaya Sarah Chiwamba walimwambia baadhi ya nyumba za wakuu wa idara hali ya usafi haiko vizuri.

Hatua hiyo ya kufunguka kwa wafanya biashara hao mbele ya mkuu wa wilaya baada ya kukelwa na baadhi ya viongozi waliokuwa wamesimamia zoezi la usafi tarehe 25 mwezi 6 mwa huu katika soko hilo walikataa kuwaandika majina baadhi ya fanyabiashara waliofanya usafi majira ya saa 2-2:30 asubuhi na kuambiwa wamechelewa kufanya usafi wakati utaratibu wa zoezi hili lilikuwa kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 4 asubuhi.

 Wafanyabiashara wa soko kuu walimuomba mkuu wa wilya kuwachukulia hatua wakuu wa idara ambao nyumba zao ni chafu bila kujali wadhifa wa vyeo vyani huku wakisema wao zoezi la usafi wanashiriki kikamilifu na walimuunga mkona mkuu wa wilaya kwa kupunguza saa za kufanya usafi mwazo ilikuwa kuanzia saa 12-10:00 asubuhi sasa kila jumamosi kuanzia saa 12-2:00 asubuhi ili kuweza kuendelea za shughuli zao za kuhudumia jamii.



Kufuatia tukio hilo septemba 8 wafanyabiasha zaidi ya 170 waliandikiwa barua na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri Justin Monko ya wito kufika ofisini kwake septemba 9 majira ya saa 8:30 mchana na kuambiwa wanatakiwa kulipa faina ya kila mtu shilingi 50,000/=.

Wafanyabiashara hao hawakuafi kulipa huku wakidai zoezi hilo ni mpango maalum kwani walisema siku hiyo walishiriki zoezi la usafi lakini viongozi waliosimamia usafi huo walikuwa wanaandika majina kwa upendeleo na hawakuwa maeneo husika wao walipokuwa wanafanya usafi.


Kwa upande wa mkuu wa wilaya Chiwamba alisema malamiko ya wafanyabiashara ameyapokea na atayashughulikia huku akiongeza kusema  hii wiki yake ya kwanza kushiriki na wananchi kwenye zoezi la usafi kwakuwa kipindi cha awali alikuwa na majukumu ya kikazi hakuweza kushiriki na zoezi hilo sasa wiki ijayo litaendeshwa mitaani ili kuhakikisha kila mwananchi anafanya usafi na kupende usafi.



Kamera za mtandao huu leo septemba 10 zilimulika baadhi ya nyumba za wakuu wa idara zilizopo kata ya Likongowele Liwale mjini mtaa maarufu unaofahamika Majumba 7 na kukuta baadhi ya nyumba hazina uzui, uchanja wa vyombo wala shimo la takataka na hazifagiliwe.

Hata hiyo kulalamikiwa kwa nyumba za watumishi hazifanyiwi usafi mtandao huu uliwahi kuandika kama maeneo hayo hali ya usafi hayarizishi >>bofya hapa  kuangalia taarifa iliyowahi kuandikwa 

Post a Comment

 
Top