0

Zari la Ngassa lamuangukia Kiiza

Siku moja baada ya mkataba kati ya Mrisho Ngassa na Free State Stars ya Afrika Kusini kuvunjwa, klabu hiyo imemsajili mshambuliaji wa zamani wa Simba na Yanga, Hamis Kiiza.

Msimu uliopita, Kiiza raia wa Uganda aliitumikia Simba na kufunga mabao 24 katika michezo yote msimu uliopita kabla ya klabu hiyo kutangaza kumtema katika usajili wa msimu huu.

Taarifa iliyotolewa na timu ya Free State Stars na kunukuliwa na mtandao wa Kickoff.com, zimethibitisha usajili wa mshambuliji huyo, ambaye pia huchezea timu ya Taifa ya Uganda.

“Kiiza amesaini kuichezea Free State juzi, ni mchezaji ambaye msimu uliopita alicheza Simba,” kilisema chanzo hicho na kubainisha kuwa mchezaji huyo alisaini mkataba wa miaka miwili.

Post a Comment

 
Top